Mkuu
wa Wilaya ya Monduli, Idd Kimanta amewataka wananchi wanaochunga mifugo
eneo linalotumika kwa mafunzo ya kijeshi kutoa taarifa kwenye kambi za
Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) ili kuepusha vifo.
Kimanta
alitoa kauli hiyo jana katika Kijiji cha Nafco, Kata ya Loksale wakati
wa maziko ya watoto watatu waliopoteza maisha wakichunga mifugo ya
familia kwenye eneo la mafunzo ya jeshi la Loksale wilayani hapa, Ijumaa
iliyopita.
Watoto
hao; Johnson Daniel Mollel ambaye ni mwanafunzi wa darasa la tatu
katika Shule ya Msingi Nafco, Emmanuel Saitabau Mollel wa darasa la
kwanza na Samweli Nyangusi walipoteza maisha wakati wakichunga baada ya
kulipuliwa na bomu.
Kimata
alisema kwa muda mrefu kumekuwa na ushirikiano kati ya kambi za JWTZ
zilizopo wilayani humo na vijiji vinavyozunguka maeneo ya mafunzo, hivyo
tukio hilo ni la bahati mbaya.
Brigedia
Jenerali Rajab Hunt kutoka Kambi ya Monduli alisema tukio hilo
halikutarajiwa kwa kuwa Serikali inanunua silaha kwa ajili ya ulinzi na
si kuwadhuru wananchi.
Mkuu
wa Brigade ya Mbuni, Brigedia Jenerali Athanas Mbonye alisema wananchi
wasiwe na wasiwasi kwa sababu jeshi lipo kuwalinda na watoe taarifa
wanapoona vifaa wanavyovitilia shaka.
Kiongozi
wa mila wa jamii hiyo ya wafugaji, Loibanguti Loondawa alisema tukio
hilo limeleta majonzi kwa familia na ni la bahati mbaya kwa kuwa
halikuwa limekusudiwa.
Oktoba,
2012 watoto watano wakiwamo watatu wa familia moja walikufa kwa
kulipukiwa na bomu wilayani Karagwe mkoani Kagera walipokuwa
wakilichezea baada ya kuliokota kwenye vyuma chakavu.
chanzo:Mpekuziblog.
Comments