
Kwa mujibu wa taarifa ya ikulu, rais dk shein amemteua Amour Hamad
Saleh kuwa ofisa mdhamini ofisi ya rais na mwenyekiti wa baraza la
mapinduzi-pemba.
Bibi Sabra Issa Machano ameteuliwa kuwa mkurugenzi mwendeshaji wa
mfuko wa hifadhi ya jamii Zanzibar (ZSSF), Bibi Salama Ramadhan makame
ameteuliwa kuwa kamishna wa idara ya watendakazi katika tume ya mipango
zanzibar.
Aidha Seif Shaaban Seif ameteuliwa kuwa kamishna wa idara ya mitaji
ya umma, Othman Juma Othman anakuwa mkurugenzi mtendaji wa mamkala ya
ununuzi na uondoaji wa mali za serikali.
Wengine ni Rashid Mohamed Kassim aliyeteuliwa kuwa mkaguzi wa ndani
mkuu wa hesabu za serikali, khamis shibu mwalimu mkurugenzi wa idara ya
sera za kodi na fedha katika wizara ya fedha na mipango.
Mohammed Jaffar Jumanne ameteuliwa kuwa mkurugenzi wa idara ya
uendeshaji na utumishi katika wizara ya biashara, viwanda na masoko,
khamis ahmada shauri, mkurugenzi wa idara ya biashara na masoko.
Wengine ni dkt vuai iddi lila ameteuliwa kuwa katibu mtendaji wa
kamisheni ya utalii, zahor kassim mohamed anakuwa
mkurugenzi mwendeshaji wa kampuni ya uvuvi ya zanzibar (zafico).
Asha hamid rajab ameteuliwa kuwa mthamini mkuu katika wizara ya
ardhi, maji, nishati na mazingira na ali suleiman ameir anakuwa
mkurugenzi wa idara ya ajira katka wizara ya kazi, uwezeshaji, wazee,
vijana, wanawake na watoto.
Uteuzi huo unaanza jumatatu septemba 25, 2017
Imetolewa na habari maelezo zanzibar
23 septemba 2017.
chanzo: zanzibar24.
Comments