Licha ya kuwepo kwa sheria ya makosa ya mtandao, usambazaji wa taarifa za uongo mitandaoni umeendelea kuwa changamoto sugu.
Kutokana
na hali hiyo, kitengo cha polisi cha makosa ya mtandao kinaendelea
kufanya doria mitandaoni ili kuwabaini wahusika hao na wengine wa makosa
ya mtandao.
Joshua
Mwangasa, naibu mkuu wa kitengo hicho amesema hayo leo Ijumaa wakati wa
uzinduzi wa awamu ya pili ya kampeni ya matumizi sahihi ya mitandao ya
kijamii.
Amesema kuna kesi nyingi za watu kusambaza taarifa za uongo kwa makusudi na wengine bila kufahamu kuwa ni kosa kisheria.
"Hatuingilii
mawasiliano binafsi, sisi tunachunguza yale ambayo yanawafikia
wanajamii, huko tunagundua wapo wanaofanya kwa makusudi na wengine
hawafahamu kama ni kosa kisheria, lakini kutojua sheria si utetezi,"
amesema Mwangasa.
Mmiliki
wa Blogu ya Fikra Pevu, Maxence Melo amesema waendeshaji wa blogu
wanakabiliwa na changamoto ya watumiaji kutojua sheria.
"Wengi
hawajui hizo sheria zilizopo, utakuta mtu anaandika maoni hadi
unajiuliza alifikiria nini kuandika hiki, hii inatupa wakati mgumu
kuanza kupitia maoni ya kila mmoja. Kama huna muda ndiyo unakuta vitu
visivyofaa vinasomeka," amesema Melo.
chanzo:Mpekuziblog.
Comments