Mahakama
Kuu Kanda ya Sumbawanga mkoani Rukwa imewahukumu adhabu ya kifo watu
sita ambao ni ndugu wakazi wa Kalambo baada ya kupatikana hatia ya
kumuua ndugu yao.
Ndugu hao wamedaiwa kwamba walifikia uamuzi wa kumuua ndugu yao huyo kwa madai ya kwamba anajihusisha vitendo vya kishirikiana.
Hukumu
hiyo imetolewa jana Jumanne na Jaji Mahakama hiyo, Dk Adam Mambi baada
ya kuridhika na ushahidi uliotolewa mahakamani hapo na upande wa
mashitaka uliopeleka mashahidi sita ili kuthibitisha mashitaka hayo.
Waliokutwa
na hatia katika shauri hilo ni Ferdinand Kamande, Peter Mpandisharo,
Edes Kamande, Stephen Sikanda, Henrick Nguvumali na Anatory Kamande huku
Alistid Kamande na Will broad Kamande wakiachiwa huru kwa kutokutwa na
hatia.
Katika
shauri hilo upande wa mashitaka uliongozwa na mawakili wa serikali
ambao ni Scolastica Lugongo na Adolf Lema huku upande wa utetezi
ukiwakilishwa na wakili Mathias Budodi, ambapo ilidaiwa kwamba
washitakiwa walitenda kosa hilo Septemba 27, mwaka 2014.
Ilielezwa
mahakamani hapo kuwa siku ya tukio nyakati za usiku washitakiwa wakiwa
na silaha za jadi kama vile mapanga, nondo, mawe, majembe walivamia
nyumba ya Kamande na kugonga dirisha kisha kuvunja mlango ambapo Kamande
alikimbia kuelekea kusikojulikana.
Ilielezwa kwamba baada ya hapo waliichoma moto nyumba hiyo na kuteketeza kila kitu kilichokuwemo ndani kisha kuondoka zao.
Wakati
nyumba hiyo ikiteketea kwa moto Kamande aliyekuwa amekimbia ili
kunusuru maisha yake, alikamatwa na watu hao na kuanza kupigwa huku
wakimtuhumu kuwa ni mchawi na baada ya kumpiga sehemu mbalimbali za
mwili wake walimchoma moto na kufariki papo hapo.
Ilidaiwa kwamba washitakiwa hao walikamatwa na polisi Oktoba 10, 2014 na baada ya kuhojiwa na polisi walikana shitaka hilo.
Awali
kabla ya kutolewa kwa hukumu hiyo, mawakili wa Serikali waliiomba
mahakama kutoa adhabu kali iwe fundisho kwani watu wamekuwa wakichukulia
sheria mkononi na kuua watu kinyume cha sheria wakiwatuhumu kuwa ni
washirikina.
Akitoa
adhabu hiyo Jaji wa Mahakama hiyo, Dk Mambi amesema ameridhishwa
ushahidi uliotolewa mahakamani hapo na upande wa mashitaka hivyo kwa
kutumia Kifungu cha Sheria ya Makosa ya Jinai Namba 196 Sura ya 16 kama
ilivyofanyiwa marejeo 2002 anawahukumu watu hao sita kifo kwa kunyongwa.
chanzo:Mpekuziblog.
Comments