Hata hivyo, amesema mkakati wa Serikali ni kutaka wajulikane.
Mwigulu amesema hayo leo Alhamisi katika kipindi cha Power Breakfast kinachorushwa na Kituo cha Redio cha Clouds FM.
Amesema
katika matukio kadhaa yaliyofanywa na watu hao, polisi ilipowakamata na
kuchunguza ilibaini wawili kati yao walikuwa raia wa kigeni na wengine
ni Watanzania.
“Hatujui watu wasiojulikana wanapanga
nini, ila nawahakikishia Watanzania kuhusu usalama wao.
Tutapambana na mhalifu wa aina yoyote na tutachukua hatua mara moja bila kusita,” amesema.
Tutapambana na mhalifu wa aina yoyote na tutachukua hatua mara moja bila kusita,” amesema.
Amesema mbali ya matukio ya watu wasiojulikana
kufanya mauaji Mkuranga, Kibiti na Rufiji, aina ya watu hao ndio
wamehusika katika kumshambulia na kumjeruhi kwa risasi Mbunge wa Singida
Mashariki, Tundu Lissu.
Amesema polisi wanaendelea
kuchunguza kila taarifa inayohusu mazingira ya tukio hilo lililotokea
Septemba 7 ijapokuwa kwa sasa asingependa kuzungumzia hatua iliyofikiwa
ili kutoharibu upelelezi.
chanzo:mwananchi.
chanzo:mwananchi.
Comments