Mwigulu: Aliyemtisha Nape Kwa Bastola Sio Askari Polisi, Uchunguzi Sakata la Beni Saa Nane Bado Unaendelea.
Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba, amesema aliyemtishia
bastola aliyekuwa Mbunge wa Mtama, Nape Nnauye, hakuwa askari.
Amesema
kijana hiyo alikuwa ni mhalifu aliyetumia nafasi ya mkutano wa Nape na
waandishi habari kutaka kutekeleza tukio hilo ambapo aliishia kumtishia
bastola.
“Awali
tulidhani yule kijana ni polisi lakini hakuwa na sare za polisi, cha
kwanza nilimuelekea Inspekta Jenerali wa Polisi (IGP) kufuatilia na
akaleta majibu kuwa hakuwa polisi,” amesema Mwigulu akihojiwa na Kituo
cha Televisheni cha Clouds leo.
Aidha,
amesema suala la aliyekuwa msaidizi wa Mwenyekiti nwa Chama cha
Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe, Ben Sanane ni ngumu
kulisemea kwamba amefariki au yuko kwani polisi bado wanaendelea na
uchunguzi.
“Kwa
aina ya taarifa ninazopata ni kama inaelekea kufikia ukomo ni jambo
ambalo tumelipa uzito kulifanyia kazi na Mtanzania yeyote mwenye nia
njema anaweza kutusaidia kufuatilia,” amesema.
chanzo:Mpekuziblog.
Comments