
Mwanafunzi huyo mwenye umri wa miaka 17 anadaiwa kuionesha silaha
hiyo kwa wanafunzi wenzake ambao baadaye walimripoti kwa uongozi wa
shule.
Kwa mujibu wa hati ya mashtaka iliyowasilishwa Mahakamani hapo Polisi
wanapanga kumshtaki kwa kumiliki pistol HK45, yenye namba 25094705
kinyume na kifungu cha 34(1) cha Sheria ya Silaha za moto.
Mwanafunzi huyo aliwaambia wapelelezi kuwa aliipata silaha hiyo
kutoka kwa ndugu yake aliyekuwa anaishi Marekani ambaye sasa ni
Mkurugenzi wa Jaramogi Oginga Odinga University ingawa ripoti
zilizowasilishwa Mahakamani zimedai aliichukua silaha hiyo chumbani kwa
ndugu yake huyo katika Kaunti ya Siaya.
chanzo: zanzibar24.
Comments