Takribani
familia 13 zenye jumla ya watu 44 za Polisi zimekosa makazi baada ya
nyumba walizokuwa wakiishi kuteketea kwa moto jana usiku majira ya saa
moja.
Nyumba
hizo wanazoishi polisi zilizopo katika kata ya Sekei Jijini Arusha
zimeeketea kwa moto na chanzo cha ajali hiyo kutajwa kuwa ni hitilafu ya
umeme.
Mkuu
wa Kikosi cha Zimamoto na Uokoaji mkoani Arusha, Andrew Komba alieleza
kuwa kama siyo taarifa kuchelewa kulifika jeshi la zima moto, basi
huenda wangeweza kuokoa mali nyingi zaidi.
“Tungefika mapema nusu ya nyumba zilizoteketea tungeziokoa,” amesema Komba.
Aidha
Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo ambaye naye alifika katika eneo la
tukio alilipongeza Jeshi la zima moto kwa juhudi kubwa walizozifanya
kuuzima moto huo na kuokoa maisha ya watu pamoja na mali.
“Kuna
Nyumba za watumishi wetu askari zimepata ajali ya kuungua moto.
Nichukue fursa hii kuwapongeza jeshi la zima moto kwa juhudi kubwa ya
kuhakikisha kuwa wamezima moto huu. Takribani familia 13 zimeathirika
kutokana na ajali hii ambazo zina watu kama 44….. Taarifa za awali
zinaeleza kuwa ajali hii imetokana na hitilafu ya umeme..,” alisema RC
Gambo.
Naye
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Charles Mkumbo amesema kuwa tukio
hilo ni janga, hivyo watakaa kuona ni kwa namna gani watawasaidia
walioathiriwa.
chanzo:Mpekuziblog.
Comments