Mkarafuu wampa jeraha Pemba.

Mkaazi wa Kizimbani Wilaya ya wete Rashid Ali Suleimani Amefikishwa  Hospitali ya Wete kwa matibabu baada ya kuanguka kutoka juu ya mkarafuu huko katika bonde la tungamaa.

Tukio hilo limetokea juzi majira ya saa tisa za jioni wakati kijana huyo alikuwa katika harakati za kuchuma karafuu.

Shuhuda wa Tukio hilo Khatib Omar Khatibu amefahamisha kuwa alisikia kelele kutoka kwa watu waliokuwa karibu nae na baada ya kufika alimkuta akiwa ameanguka na kuanza harakati za umfikisha Hospitali.
Kwaupande wa taarifa kutoka kwa Daktari ambae amethibitisha tukio hilo Suleiman Bakari amesema kuwa majeruhi ameumia zaidi katika sehemu za mgongo “Tumefanya uchunguzi pamoja na kumfanyia uchunguzi wa mgongo napia kubaini pia amepata majeraha katika sehemu ya mguu”
Ndugu najamaa wa majeruhi huyo hapojana walikuwa wanaharakati za kumsafirisha katika Hospitali kuu ya Mnazi mmoja kwa ajili ya kupata matibabu zaidi.
chanzo:zanzibar24.

Comments