Mwenyekiti
wa Chadema, Freeman Mbowe amewashukuru Watanzania wanaoendelea
kumchangia Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu akiwataja
wanaoongoza katika kuhamasisha uchangiaji mitandaoni akiwamo Mange
Kimambi na Wema Sepetu.
Mbowe
amesema mpaka leo Ijumaa jumla ya Sh204 milioni zimepatikana katika
michango hiyo pamoja na msaada wa hali ambao wamekuwa wakipewa na
Watanzania.
“Tunawashukuru
wanaoendelea kuchangisha, tunamshukuru Mange Kimambi kwa kuwahamasisha
diaspora kuchangia na katika mitandao akishirikiana na Wema Sepetu na
wengine,” alisema Mbowe.
Mange
alianzisha kampeni ya kumchangia Lissu katika mtandao wa Gofundme
akilenga kupata dola za Marekani 50,000 na mpaka kufikia leo saa 10.41
katika mtandao huo kiasi cha dola za Marekani 23,380 ilikuwa imepatikana
ambayo ni wastani wa Sh51.3 milioni.
chanzo:Mpekuziblog.
Comments