Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja, Hassan Nassir Ali amesema kuwa kijana huyo ambaye ni mkaazi wa Kiembe Samaki mwili wake umeokotwa majira ya saa 12 asubuhi katika eneo la bustani ziliopo katika mtaa wao wa Kiembesamaki.
Kamanda huyo amesema kuwa kuokotwa kwa mwili huo kunatokana na taarifa kutoka kwa wananchi juu ya kuwepo kwa mwili huo katika eneo hilo ambalo ni kawaida ya wananchi kufika kwa ajili ya kubadilishana mawazo kutokana na kuwa ni sehemu ya utulivu.
Amesema kwa mujibu wa taarifa za awali wamebaini kuwa kijana huyo inadaiwa kuwa na tabia ya wizi kwa muda mrefu hali ambayo inaonekana kuwa chanzo cha kukumbwa na tukio hilo kutoka kwa watu wasiojulikana.
Aidha ameongeza kuwa, pamoja na hali hiyo lakini bado Jeshi hilo halijabaini nani au kundi gani linahusika na tukio hilo la kumcharaza mapanga kijana huyo hadi kupelekea kupoteza maisha.
Pamoja na hayo, Kamanda Nasir ameitaka jamii kuacha tabia ya kuchukua sheria mikononi mwao na badala yake wawafikishe kwenye vyombo vya sheria wale wote wanaobainika kuhusika na matendo mbali mbali ya uvunjifu wa amani katika jamii.
Hata hivyo amesema mwili wa kijana huyo tayari umekabidhiwa kwa ndugu na familia yake kwa ajili ya hatua ya mazishi, ambapo tayari ameshazikwa.
chanzo:zaimamedia.
Comments