Mbunge wa Singida Kaskazini(CCM), Lazaro Nyalandu amesema kwamba madaktari wa Kenya wamesema Tundu Lissu hawezi kusafirishwa kwenda nje kwa ajili ya kumpatiwa matibabu.
Mbunge
Nyalandu ameeleza hayo kwenye ukurasa wake wa Instagram, Facebook na
Twitter kwamba mipango ya kumsafirisha Lissu ambayo walikuwa
wanafanya itasimama kwa sasa kutokana na ushauri wa madaktari hao ili
kuruhusu kukamilishiwa huduma za tiba ambazo tayari ameanzishiwa, hadi
hapo itakavyoshauriwa vinginevyo.
Katika kurasa zake
hizo za mitandao ya kijamii Nyalandu ameandika hivi, “Tunafahamu kwamba,
tangu Alhamisi, Septemba 7, siku ambayo Mh #TunduLissu, Mb., (Singida
Mashariki-CHADEMA) alishambuliwa kwa kupigwa risasi mjini DODOMA,
Watanzania wengi wamesononeshwa na kulia sana, na kubwa zaidi, WOTE
wameungana katika kuomba Sala na Dua kwa ajili ya Mh #TunduLissu, ili
mkono wa Mkombozi, aliye MUNGU wetu, upate kumgusa tena na kumponya
dhidi ya majeraha, maumivu na mateso anayoyapitia,”
“Mapema
leo(jana), baada ya kutembelea #Nairobi Hospital asubuhi, nimefanya
mazungumzo mchana wa leo na Mh #FreemanMbowe, ambapo kwa pamoja
tumeelezwa kuwa MADAKTARI #NairobiHospital wameendelea na kumtibu Mh
#TunduLissu, ikiwa ni pamoja na kuanza upasuaji, na huduma zingine za
Kitabibu walizomwanzishia tangu awasili Nairobi siku ya Alhamisi,
Septemba 7.
IMEELEZWA vilevile kuwa kwa sasa Mh #TunduLissu ataendelea na TIBA hospitalini hapo kutokana na kile kilichoelezwa kuwa hali yake bado ni "Critical but stable", na KWAMBA mwili wake unaendelea kuitikia vema matibabu lukuki anayofanyiwa kwa wakati mmoja,”
IMEELEZWA vilevile kuwa kwa sasa Mh #TunduLissu ataendelea na TIBA hospitalini hapo kutokana na kile kilichoelezwa kuwa hali yake bado ni "Critical but stable", na KWAMBA mwili wake unaendelea kuitikia vema matibabu lukuki anayofanyiwa kwa wakati mmoja,”
“KWA
SASA, mipango ya kumsafirisha Mh #TunduLissu NJE itasimama, kutokana na
ushauri wa MADAKTARI #NairobiHospital, ili kuruhusu kukamilishiwa
huduma za TIBA ambazo tayari ameanzishiwa, hadi hapo itakavyoshauriwa
vinginevyo, ama endapo kutatokea umuhimu wa kufanya hivyo katika SIKU
zijazo,”
“AIDHA, SOTE tuzidi KUMWOMBEA MUNGU na kushiriki katika CHANGIZO za kusaidia gharama za matibabu yake,”
“NI
DHAHIRI kwamba Wana Singida, na Watanzania WOTE tumeumia, tumekwazwa,
na tumesononeshwa sana kwa uonevu na dhuluma aliyotendewa ndugu yetu Mh
#TunduLissu. Kitendo hiki hakikubaliki mbele za MUNGU na mbele za
wanadamu,”
“Tunaiomba Serikali yetu iendeleze juhudi
zake na kuchukua hatua za haraka kuwasaka, kuwakamata, na kuwatia
mbaroni watu wote waliohusika kupanga na kutekeleza shambulio hili la
kigaidi dhidi ya Mh #TunduLissu. Aidha, shambulio hilo walilolifanya
watu wasiojulikana limedhalilisha taifa, na kudhoofisha taswira ya
kukomaa kwa demokrasia inayoruhusu kuvumiliana na kuheshimiana licha ya
tofauti zetu za kiitikadi na mitazamo ya kisiasa,”
“HALIKADHALIKA,
kwetu sote kama TAIFA, huu ni wakati wa Watanzania wote kuwa wamoja,
bila kujali tofauti zetu za kiitikadi, kidini, wala kikabila, tuungane
na kulaani kitendo hiki na vitendo vyote vya uonevu na kuumizana. TANGU
zamani, IMEANDIKWA: Haki HUINUA Taifa.”
chanzo:Mwananchi.
chanzo:Mwananchi.
Comments