Katibu
Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Sharif Hamad, ameeleza
maendeleo ya afya ya Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu (Chadema),
baada ya kumtembelea hospitalini Nairobi, Kenya.
Akihojiwa
na Redio ya Idhaa ya Kiswahili Deutsche Welle (DW) ya Ujerumani jana,
Maalim Seif alisema Lissu anaendelea vizuri na hajapoteza mwelekeo.
“Jana
(juzi) nilimtembelea Lissu na nilipata moyo sana, kwa kweli anaendelea
vizuri ukizingatia mtu ambaye alipigwa risasi zaidi ya 30, anapata nafuu
haraka haraka.
“Bado
hajapoteza mwelekeo akili yake ipo timamu, ametuhakikishia haya
yaliyotokea hayatamrudisha nyuma katika kuwatetea wanyonge.
“Anazungumza vizuri, yuko makini sana anajua anachokisema na mimi nimepata moyo jinsi nilivyomuona,” alisema Maalim Seif.
Alisema kutokana na mambo yanayoendelea nchini, lazima kuwapo na mjadala wa taifa kuona tumekosea wapi na kujirekebisha.
“Mambo
kama haya kutokea Tanzania ni jambo ambalo kila Mtanzania lazima
aingiwe na wasiwasi kwa sababu hakuna hata mmoja na hasa mwanasiasa
ambaye ana usalama wa maisha yake.
“Kama taifa tuzungumze kuona tumekosea wapi na kujirekebisha,” alisema.
Kuhusu
uchunguzi wa tukio hilo, alisema hata kama vyombo vya dola vya ndani
vitafanya si aibu kwa nchi kutafuta msaada kwa wengine.
“Yako
mambo mengine yaliyotokea huko nyuma na bado hatujaaambiwa yalikwenda
vipi, tunaambiwa tu uchunguzi unaendelea. Ni vizuri wananchi waone
matokeo ya uchunguzi huo…si aibu kwa nchi kutafuta msaada kwa wengine,”
alisema.
Lissu
alipigwa risasi zinazokadiriwa kufikia 32, Septemba 7, mwaka huu,
alipokuwa akirejea nyumbani kwake Area D mjini Dodoma baada ya kutoka
kuhudhuria kikao cha Bunge na kujeruhiwa vibaya sehemu mbalimbali za
mwili wake.
chanzo:Mpekuziblog.
Comments