Mbunge wa Iringa Mjini (Chadema),
Mchungaji Peter Msigwa amesema hali ya Mbunge wa Singida Mashariki,
Tundu Lissu inaendelea vizuri na anatamani apate nafuu na kunyoosha
vidole viwili (ishara ambayo hutumiwa na Chadema).
Akizungumza
na Mwananchi katika mahojiano maalum leo Jumatano jioni jijini Dar es
Salaam, Mchungaji Msigwa amesema kwa kipindi chote hicho Lissu hakuwa
akila na hali yake imebadilika ukilinganisha na alivyokuwa hapo awali
lakini hivi sasa anakula vitu laini.
“Leo kabla
sijaanza safari ya kuja (kurudi Dar es Salaam) amenitania sana kwa
kusema anatamani apate nafuu na kuonyesha alama ya vidole viwili,”
amesema Mchungaji Msigwa.
Msigwa ameeleza wanaendelea kujadiliana na madaktari ili kuangalia uwezekano wa kumpeleka nchi nyingine kwa ajili ya matibabu zaidi.
Amesema Lissu anaangaliwa na madaktari 10 kila mmoja akishughulika na eneo lake ili kuhakikisha hali yake inatengemaa.
“Miongoni mwa mambo anayoyarudia ni kututaka kuendelea kupambana, kupaza sauti kuikomboa nchi, ”amesema Msigwa.
chanzo:Mwananchi.
chanzo:Mwananchi.
Comments