Akizungumza
kwa simu na Mwananchi leo Jumanne, Kubenea amesema yupo katika kituo
cha polisi cha Oysterbay wilayani Kinondoni na akisubiri utaratibu wa
safari ya kwenda Dodoma kwa ajili ya kuhojiwa kama Spika wa Bunge Job
Ndugai alivyoagiza.
Kubenea amesema awali kabla ya
kushikiliwa alikwenda kujisalimisha polisi katika kituo hicho kisha
aliambatana na askari hadi Katika Hospitali ya Aga Khan ambako alitakiwa
kwenda kwa ajili ya kufanyiwa kipimo cha MRI.
“Baada
ya kipimo kukamilika daktari alishauriwa nipumzike, lakini askari
wakaamuru niondoke na kurudi Oysterbay. Hapa ninapozungumza na wewe nipo
kituo nikisubiri kusafirishwa kwenda Dodoma,”amesema Kubenea na
kuongeza kuwa;
“Hata hivyo, daktari ameshauri
nisisafiri kwa njia ya barabara kutokana na matatizo ya mgogo niliyokuwa
nayo hivyo nasubiri utaratibu hapa,” amesema mbunge huyo.
Akizungumzia
kushirikiliwa kwa Kubenea, Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalumu ya Dar es
Salaam, Lazaro Mambosasa amesema jeshi hilo lilikuwa na hati ya
kukamatwa kupelekwa Dodoma kwa mbunge huyo ndiyo maana yupo mikononi
mwao.
“Atapelekwa lini, atatoka saa ngapi au
atasafirishwa kwa njia gani hilo mimi sijui ila atapelekwa Dodoma chini
ulinzi wa polisi. Ukishakuwa na hati ya kukamatwa lazima utakaa mahabusu
tu,”amesema Kamanda Mambosasa.
Hata hivyo, Kamanda Mambosasa amesema;“Kwanza sijui kama yupo polisi ndiyo kwanza nakisikia kwako,” alieleza.
Alipotafutwa
mwenyekiti wa kamati hiyo, George Mkuchika kujua kama wajumbe wajumbe
kamati yake, bado wapo Dodoma baada ya kikao cha Bunge kuhairishwa wiki
iliyopita alijibu;
“Shughuli za kamati yangu
hazifanyika katika magazeti, sisi tunafanya kimyakimya kisha
tunamkabidhi Spika wa Bunge,” alijibu Mkuchika kisha kukata simu.
chanzo:Mwananchi.
Comments