Kitimtim cha Wanafunzi kuchagawa skuli chaikumba Sekondari Unguja.

Mwalimu Mkuu Skuli ya Mwera Sekondari Mbarak Omar Ali Uvumilivu umemshinda kutokana na wanafunzi kuchagawa na kuamua kuwaita baadhi ya wazee wakamati ili kutafuta ufumbuzi wa matatizo hayo.

Amesema kuwa Suala la kuchagawa linamtowa mudi wanafunzi  kwani anakuwa hana akili ya kibinadamu na haswa katika kipindi cha mitihani inakuwa ni vigumu kufanya mtihani kwasababu hawezi kutumia akili yake timamu.


Kwaupande wa viongozi wa kamati wa Skuli hiyo Mzee Salmini Jecha amesema kuwa “hakuna budi  wazazi wa wanafunzi hao kuwa pamoja na kamati ya Skuli na kamati ya walimu kwasababu hatujuwi back ground ya vijana hao kwani  mmoja miongoni wao yanapomfika mambo hayo tu akiingia darasani wenziwe wanakuwa wanachagawa nilazima tukae pamoja na wazazi na kuweza kuomba dua sio kuanza kutafuta vitu vyakuchinja na kuanza kumwaga damu”
Endapo wazazi kamati na walimu ikiwa watashirikiana tatizo hili linaweza likaondoka.

chanzo:zanzibar24.

Comments