Naibu
Waziri wa Afya, Dk Hamisi Kigwangalla ameiagiza Taasisi ya Kuzuia na
Kupambana na Rushwa (Takukuru) kumkamata tabibu, Daniel Mtatiro wa kituo
cha afya Kiagata anayetuhumiwa kula Sh2 milioni za Mfuko wa Afya ya
Jamii (CHF).
Dk
Kigwangalla aliye katika ziara mkoani Mara amekagua zahanati, vituo vya
afya na hospitali ikiwa ni katika mpango wa kuboresha sekta ya afya.
Baada
ya kufanya ziara katika kituo hicho cha afya, Dk Kigwangalla amemwagiza
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Butiama mkoani Mara, Simon
Ngiliule kumsimamisha kazi mara moja kutokana na tuhuma hizo.
Pia, ameiagiza Takukuru kumkamata tabibu huyo ili kuhojiwa na kuchukuliwa hatua.
"Nakuagiza
mkurugenzi msimamishe kazi Mtatiro na afikishwe Takukuru haraka sana.
Huku ni kuhujumu mpango wa Serikali wa kuwaletea maendeleo kupitia afya
matokeo yake mtu mmoja anachukua fedha za wananchi mwishowe wanakosa
matibabu," alisema Dk Kigwangalla.
chanzo:Mpekuziblog.
Comments