Wananchi wa Jimbo la Kikwajuni wamesema wamefurahishwa na hatua za viongozi wao wa jimbo hilo kwa kulipa umuhimu suala la matibabu ambapo limeweza kuwapunguzia usumbufu wa kufata huduma za afya nje ya Zanzibar.
Miongozni mwa Magonjwa yanayotibiwa ni mifupa,Presha,Sukar,Uti wa mgongo ambapo matibabu yake yatakuwa bure pamoja na upatikanaji wa dawa bila ya malipo.
Wakizungumza mara baada ya kupatiwa huduma za afya katika eneo la Rahaleo baadhi ya wananchi hao Amina Abrahmani,Juma Ali Kitwana wamesema ujio wa madaktari bingwa katika jimbo lao umeweza kuleta faraja na kusaidia wananchi kuweza kupata huduma za afya bure.
Hata hivyo wamewaomba viongozi wao zoezi hilo la matibabu kuwa endelevu kwani bado wananchi wanapata usumbufu sana katika kumudu gharama za matibabu hasa ya mifupa.
Nao Viogozi wa Jimbo hilo Mbuge Hamad Yussuf Masauni,Mwakilishi pamoja na Diwani wamesema ujio wa madaktari bingwa katika jimbo lao ni miongoni mwa ahadi zao walizoziahidi kwa wananchi wakati wakiinadi ilani ya chama cha mapinduzi.
Aidha wamewaahidi kuzitekeleza ahadi zote walizoziahidi kwa wananchi awamu kwa awamu ili kuwaondolea usumbufu wa huduma mbalimbali zinazowakabili.
chanzo;zanzibar24
Comments