Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamo wa pili wa Raisi Muhammed Aboud mohammed amelitaka Jeshi la Polisi Zanzibar kuwadhibiti na kuwachukulia hatua Viongozi wa siasa wanaoharibu amani iliopo jambo ambalo halitaleta taswira nzuri katika nchi.
Akizungumza na Viongozi wa Jeshi la Polisi katika makao makuu ya Jeshi hilo ziwani mjni Zanzibar Waziri Aboud amesema kumekuwa na wanasiasa pamoja na viongozi wanajaribu kuharibu amani katika Nchi jambo amabalo ni kinyume na Utaratibu wa kazi zao .
Aidha amesema ni vyema kwa watu hao wakatafutwa na kuchukiliwa hatua za kisheria ili kuendelea amani iliopo kwa lengo la kuepukana na athari zinazoweza kujitokeza katika jamii.
Akizungumzia suala la Uuzwaji na ,Utumiaji na Usambazaji wa Dawa za kulevya Waziri Aboud amelitaka Jeshi la posi kuengeza kasi katika kupambana dawa za kulevya katika jamii ili kuondoa tatizo hilo linalochangia kupoteza vijana ambao ni nguvu kazi ya taifa.
Amesema mbali na jitihada zinazofanywa katika kudhiti suala hilo lakini bado watu wanaendelea na uuzaji na usambazaji wa dawa za kulevya katika jamiia na kusababisha athari mbali mbali ikiwemo kuenea kwa vitendo vya kihalifu vinavyofanywa na watumiaji wa dawa za kulevya.
Kwa upande mwengine waziri Aboud ametowa wito kwa Jeshi hilo kuandaa mikakati ya kudhibiti vitendo vya udhalilishaji na Unyanyasaji wa kijinsia vinavyoendea katika jamii ikiwemo kusimamia ipasavyo ushahidi unaotolewa katika kesi ili kesi hizo ziwee kupatiwa ufumbuzi kwa wakati.
Awali Akisoma Taarifa ya hali ya usalama hapa Zanzibar kuazia Januari hadi Agosti mwaka huu Kaimu kamishna wa Jeshi la polisi Polisi Juma Yussuf Ali amesema hali ya usalama inarizisha licha ya kuwa na matatukio mbali mbali yanayojitokeza ikiwemo kuwepo kwa vitendo vya Wizi,Uuzaji na Usambazaji wa dawa za kulevya pamoja na kuwepo kwa mauaji yanyosababishwa na wananchi kujichukulia hatua mikonini mwao.
Amesema Jeshi la polisi linaendelea na jitihada za kupambana na vitendo hivyo ili wahusika waweze kuchukuliwa hatua za kisheria pamoja na kuendelea amani iliopo katika jamii.
Hata hivyo Naibu kamishna huyo amesema licha ya kuwa wanaendelea kufanya kazi kwa uadilifu lakini wanakabiliwa na matatizo mbalimbali katika kutekeleza majukumu yao ikiwemo ukosefu wa makaazi kwa askari pamoja na uhaba wa vitendea kazi kama vile boti za doria jambo ambalo linapelekea kushindwa kutekeleza majukumu yao kwa wakati.
chanzo:Zanzibar24.
Comments