
Kikao hicho cha kawaida kimefanyika kwa mafanikio makubwa katika ukumbi wa Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui Zanzibar.
Kwa mujibu wa taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa na Katibu wa Kamati Maalum ya NEC, Idara ya Itikadi na Uenezi Zanzibar Ndg Waride Bakari Jabu, pamoja na mambo mengine kilipokea
na kujadili majina ya wagombea 50 waliojitokeza kuomba nafasi za
Uenyeviti CCM Wilaya 12 za Unguja na Pemba na kutoa mapendekezo yake
ili kuyapeleka katika vikao husika.
Aidha kikao hicho kilimpongeza Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar,
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi kwa kufanya ziara
ya Chama na Serikali kwa wakati mmoja kufuatilia Utekelezaji wa Ilani
ya CCM ya mwaka 2015-2020 Unguja na Pemba kwa mafanikio makubwa .
Kwa upande wake Rais za Zanzibar aliwashukuru viongozi, watendaji na
wananchi mbalimbali walioshiriki katika ziara yake na kusisitiza juu
ya umuhimu wa viongozi wa Chama na Serikali kuteremka chini kwa
wananchi na kushirikiana nao katika harakati za maendeleo kubaini
changamoto zilizopo na kazipatia ufumbuzi .
Dk Sheni alimalizia kwa kusema viongozi wa Chama na Serikali wana
wajibu mkubwa wa kutimiza wajibu wao kikamilifu katika kukiwezesha
Chama na Serikali kuendelea kukubalika zaidi kwa wananchi na kushinda
kwa kiwango cha juu zaidi katika uchaguzi mkuu ujao.
chanzo:Zanzibar24.
Comments