Makamu
Mwenyekiti wa Baraza la Vijana CHADEMA taifa (BAVICHA), Patrick ole
Sosopi amefunguka na kusema wao kama chama wameamua kuwakutanisha
wanachama wao mbalimbali wa imani tofauti kwa ajili ya kufanya maombezi
ya kitaifa kumuombea Mbunge Lissu.
Akiongea
na waandishi wa habari leo Makao Makuu ya CHADEMA, Sosopi amesema kuwa
jambo hilo halihusiani na mambo ya kisiasa bali wameamua kukutana kwa
lengo la kuombea taifa katika mambo mbalimbali ikiwa pamoja na kuliombea
jeshi la polisi ili wafanye kazi zao kwa kufuata misingi ya haki na
usalama zaidi.
"Madaktari
wamefanya kazi kubwa sana kuendelea kuokoa maisha ya Tundu Lissu na
sisi tumekaa na kufikiri kwamba ni bora tukutane ili kwa pamoja tuweze
kufanya maombezi, tunajua chama chetu kina kila aina ya watu wenye imani
mbalimbali ya dini, hivyo Baraza tumeandaa maombo maalum kwa ajili ya
Mhe. Tundu Lissu na kuita 'Tanzania National youth Prayer for Lissu'
tutafanya maombi hayo ya kitaifa na kutoa wito kwa watu wote, jambo hili
si la kisiasa na wala halina sura ya kisiasa " alisisitiza Sosopi
Aidha
Sosopi amesema kuwa wanategemea kufanya maombezi hayo siku ya Jumapili
jijini Dar es Salaam maeneo ya Sinza Darajani viwanja vya TP na kudai
kwamba mpaka sasa wamefanya maandalizi yote ikiwa pamoja na kuandika
barua kwa taasisi zote za dini kuweza kufika kwa ajili ya maombezi hayo.
Mbali
na hilo Sosopi amedai kuwa kwa kuwa wanaamini jambo hilo halina sura ya
kisiasa hivyo wanategemea kuona jeshi la polisi nchini likifika kwa
lengo la kutoa ulinzi kwa raia ambao watafika kwa ajili ya maombezi hayo
na si vinginevyo.
"Naomba
jambo hili lisitafsiriwe vibaya sisi, kama viongozi wa kisiasa
tutakwenda pia kusikiliza maombi na si kwenda kuongea chochote,
tutakwenda uwanjani kwa sababu sisi kama CHADEMA hatuna kanisa wala
msikiti kufanya maombezi hayo ndiyo maana tunakwenda uwanjani hapo,
tunaamini hapo ni sehemu sahihi kuweza kuwakutanisha watu wetu wote bila
kujali itikadi zao" alisema Sosopi
chanzo:Mpekuziblog.
Comments