Chama
Cha Mapinduzi (CCM) kimempongeza mwanachama wake aliyejitolea kudhamini
ndege iliyomsafirisha Mbunge wa Jimbo la Singida Mashariki, Tundu Lissu
kwenda jijini Nairobi nchini Kenya kwaajili ya matibabu.
Katika
taarifa hiyo, imesema kuwa wamechukua hatua hiyo ya kumpongeza Mbunge
wa Jimbo la Mpendae, Salim Hassan Turky kwa kuonyesha upendo, utu na
mshikamano na kuweka kando tofauti za kisiasa.
“Kwa
dhati kabisa tunampongeza mwanachama wetu na mbunge wa Jimbo la
Mpendae, kwa kuonyesha utu na kuweka kando itikadi za kivyama kumsaidia
Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu,” amesema Polepole kupitia
taarifa hiyo
Hata
hivyo, Polepole ameongeza kuwa wameamua kumpongeza mbunge huyo kwa
kuonyesha uzalendo wa hali ya juu, kwani katika matatizo ni vyema
itikadi za kisiasa zikawekwa pembeni ili kuweza kutatua kile ambacho
kinakuwa kinawakabili.
Comments