Ofisi
ya Bunge imesema fedha zilizochangwa na wabunge Sh.43 milioni kwa ajili
ya kusaidia matibabu ya Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu
zimetumwa katika akaunti ya Hospitali ya Nairobi anakopatiwa matibabu.
Bunge
limetoa taarifa kwa umma leo Ijumaa saa chache baada ya Mwenyekiti wa
Chadema, Freeman Mbowe kuzungumza na waandishi wa habari jijini Dar es
Salaam na kueleza fedha hizo hazijatumwa.
Katika
taarifa hiyo, Bunge limesema fedha hizo zimetumwa Septemba 20 kupitia
Benki ya Barclays, Tawi la Hurlringham katika akaunti namba 045 1155318
yenye jina Kenya Hospital Association.
“Fedha
hizi zingeweza kutumwa mapema zaidi isipokuwa mawasiliano yalikuwa
yanafanyika kupata namba ya akaunti ya kutuma fedha hizo na taratibu
nyingine za malipo nje ya nchi,” imesema taarifa ya Bunge.
Ofisi
ya Bunge imewaomba Watanzania kila mmoja na imani yake kuendelea
kumuombea Lissu ili apone haraka na kurejea nchini kuendelea na majukumu
yake.
Baada
ya Lissu kushambuliwa na kujeruhiwa kwa risasi Septemba 7 nyumbani
kwake Area D mjini Dodoma akitokea bungeni, wabunge waliazimia kutoa
nusu ya posho zao kugharimia matibabu.
==>Taarifa ya Bunge
chanzo:Mpekuziblog.
Comments