Bulembo
aliwahi kusema kuwa hatogombea tena lakini baadaye aliamua kuchukua
fomu. Hata hivyo Bulembo amesema aliamua kuchukua fomu ya kugombea baada
ya kupata shinikizo kutoka kwa makatibu wakuu na wazee wa jumuiya hiyo.
"Sasa
leo(Jumanne) nimewaita kuwaeleza sitagombea tena licha ya kuchukua
fomu, naamini wagombea 48 waliopatikana, kuna mmoja atatufaa kuongoza
jumuiya hii, leo ninapeleka barua kwa katibu mkuu wa chama (Abdulrahiman
Kinana) ya kumweleza dhamira yangu hii,” amesema Bulembo leo Jumanne
alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari jijini hapa.
Bulembo
amesema uchaguzi katika ngazi ya Taifa utafanyika kuanzia Novemba 20
hadi 23, wagombea wote wapo lakini yeyote aliyeanza kampeni mapema huyo
ameshajikata," amesema.
Kuhusu hoja ya kuchukua fomu
amesema haikuwa dhambi kwa kuwa kanuni za chama zinaruhusu na upo
uwezekano wa kuwa na nafasi mbili za uongozi.
"Kumekuwa
na upotoshaji kwamba, ukiwa mbunge au waziri hauwezi kugombea nafasi
nyingine, sasa hapa nina kitabu cha kanuni za mwaka 2005, 2010, 2012 na
2017 zinasema kiongozi au mbunge, waziri anaweza kugombea ila kamati kuu
ya chama itaamua inavyofaa, kama bado anahitajika atapitishwa lakini
mie sitagombea tena,”
chanzo:Mwananchi.
Comments