Kijana mmoja alieshindwa kufanya kazi kwa kujipatia riski kihalail atiwa mbaronim na Jeshi la Polisi Mkoa wa kaskazini Unguja baada ya kijipatia fedha kwa udangajifu huko Donge karange kwa madai ya kutoa ajira ya uhamiaji.
Akithibitisha kukamatwa kwa mtuhumiwa huyo Kamanda wa Polisi Mkoa wa wa Kaskazini Unguja Hasina Ramadhan Tawfiki amemtaja mtuhumiwa huyo kuwa ni Dhaharani Muhammed Khamisi mwenye umri wa miaka 20 mkaazi wa Mkokotoni Wilaya ya Kaskazini A.
Kamanda Hsina amefahamisha kuwa kabla hajafanya tukio hilo mtuhumiwa alifika katika kijiji cha Donge Karange kwa bi Maryam Rajab Bakari na kumtaka atoe shilingi laki moja ili amtafutie kazi sehemu ya uhamiaji jambo ambalo hakuweza kulifanya wala kurejesha fedha hizo huku akijua jambo hilo ni kosa lakisheria.
Bi Hsina amesema kuwa wamejitokeza watu mwenye tabia hizi kuwadanganya wananchi na kuwatapeli kwa kuwambia watapata ajira aidha Jeshi la polisi usalama na Uhamiaji au vikosi vya SMZ.
Aidha amesema “Ninawambia kwamba wananchi wote ajira za Serikali zinatolewa bure napale ambapo ajira zinatolew huwa yanatoka matangazo nawatu wanaomba nawale ambao wanabahatika kupata nafasi hiyo wanakwenda kijiunga katika ajira hizo kwani ajia za Serikali ni bure”
Mtuhumiwa huyo anatarajiwa kufikishwa mahakamani mara baada ya taratibu zitakapo kamilika.
chanzo:zanzibar24.
Comments