
Hayo yamesemwa na Wakili wa Serikali, Salimu Msemo alipokuwa
akizungumza na waandishi wa habari mjini Dodoma, ambapo aliwataja polisi
hao wa zamani waliokutwa na hatia ni wenye namba D 8656 CPL Senga
Nyembo na G 553 PC Issa Mtama washtakiwa walikutwa na meno 70 ya tembo
yenye thamani ya Sh. milioni 800.
Wengine sita waliokuwa nao wote wamekutwa na hatia ni pamoja na
Prosper Maleto, Seif Mdumuka, Amri Bakari, Said Mdumuka, Ramadhan
Athuman na Musa Mohamed.
Amesema kuwa washtakiwa hao walikutwa na kosa hilo katika eneo la
kituo cha ukaguzi cha Kauzeni lililopo Wilaya ya Kisarawe mkoani Pwani
kabla ya kufikishwa kortini na kukumbana na adhabu hiyo.
chanzo: zanzibar24.
Comments