Jeshi la Polisi Mkoa wa kusini Pemba linamshikilia kijana mmoja kwa tuhuma zakuiba Computa aina ya laptop nane kisha kuruka kwa ndege kuelekea Dubai sasa yupo mikononi mwa Polisi akiandaliwa safari yake ya kwenda mahakamani kujibu shtaka lake.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa kusini Pemba Kamishna msaidizi muandamizi wa Jeshi la Polisi Muhammed Sheikhan Muhammed amefunguka kwakusema.
“Uchunguzi mbali mbali umefanyika kwa jeshi la Polisi hadi sasa tumefanikiwa kuzipata Computa sita na bado mbili natayari tumeshazijua zipowapi na kwabahatinzuri huyu mshtakiwa tumeshamkamata kufuatia ushirikiano wa Uhamiaji baina ya Dar es salam na Zanzibar.
Amesema tukio hilo limekuja kufuatia Kijana mmoja aliekuja kisiwani Pemba na kufanya Ofisi yake yabiashara ya kuagizia bidhaa kwa kutumia mtandao ambapo alipokewa na mwenyeji huyo ndipo walipopata matatizo ya kiofisi na kuamua kufunga ofisi hiyo ndipo mtuhumiwa huyo alipoziiba Computer hizo nakwenda kuziuza.
chanzo:zanzibar24.
Comments