Achomwa kisu cha tumbo kwa kuamua ugomvi Sokoni Mwanakwerekwe Unguja.

Jeshi la Polisi lamtia mbaroni Kijana Muhammed Ramadhan Suleiman mweye umri wa miaka 30 mkaazi wa Amani Freshi kwa kosa la kumchhinja mwenziwe kama kuku wakati akiamua ugomvi na hapo hapo kufikishwa hospitali ya Mnazi mmoja kwa matibabu.
Tukio hilo limetokea jana majira ya saa kumi nanusu huko Soko kuu la  Mwanakwerekwe Unguja.

Kwamujibu wa taarifa kutoka kwa kamanda wa Polisi Mkoa wa Mjini Magharib Kamishna msaidizi muandamizi wa Polisi Hassan Nassir Ali amemtaja kijana aliechomwa kisu kuwa ni Mussa Muhammed Kombo mwenye umri wa miaka 30 Mkaazi wa melinne, kijana huyo imani imempoza kwani alikwenda kuamua ugomvi ndipo kijana Muhammed Ramadhan Suleiman mweye umri wa miaka 30 mkaazi wa Amani Freshi kumuacha mgomviwake aliefahamika kwa jina la Dosti aliamua kuchomoa kisu na kumchoma muombezi na kumuacha akiwa na hali mbaya.
Hadi sasa kwamujibu wa taarifa zilizotufikia Zanzibar24 zinasema kuwa mtuhumiwa tayari ameshatiwa mikononi mwa Jeshi la Polisi.
chanzo;zanzibar24.

Comments