Kadi hizo hazipo kwenye vituo vya
mabasi hayo muda mrefu sasa, jambo ambalo linachangia kuongezeka kwa
foleni kwenye vituo wakati wa ukataji tiketi.
Akizungumzia
suala hilo jana, Mkurugenzi Mkuu wa Mradi wa Mabasi Yaendayo Haraka
(Dart), Mhandisi Ronald Rwakatare alikiri ukosefu wa kadi hizo kwenye
vituo.
Rwakatare alisema mchakato wa kumtafuta mzabuni ambaye atakabidhiwa kusimamia utengenezaji wa kadi kwa sasa umesimama.
“Nashindwa
kuongelea zaidi jambo hili kutokana na unyeti wake, kwa sababu
umeunganishwa na mfumo wa kielektroniki na ule wa kibenki,” alisema
Rwakatare.
Alieleza kuwa lengo lao ni kupata kampuni ambayo itakapokabidhiwa mradi huo, itaweza kutolea majibu linapotokea tatizo lolote.
“Tunaomba
radhi kwa ucheleweshwaji upatikanaji wa kadi hizo, kwa kuwa ni jambo
nyeti linalohusisha suala la mambo ya fedha,” alisema Rwakatare.
Pia, alisema wapo kwenye uchunguzi kubaini sababu za idadi ya kadi zilizouzwa, ni robo tu zinatumika hadi sasa.
Naye
Ofisa Mkuu wa Operesheni Kampuni ya Max Malipo, Ahmed Lussasi alisema
awali walishinda zabuni na kupewa kazi ya kutengeneza kadi hizo, kadi
200,000 zilitengenezwa ila mradi huo haukufika mwisho na hivi sasa upo
mikononi mwa Dart wenyewe.
Ongezeko la abiria
Tangu
kuanza kwa mradi wa mabasi yaendayo haraka (BRT) idadi ya abiri imekuwa
ikiongezeka na hadi Juni, ulikuwa unasafirisha watu 200,000 kwa siku
kutoka watu 50,000 waliokuwa wakisafirisha mwaka jana baada ya mradi huo
kuanza kazi.
Kuongezeka kwa idadi hiyo inaelezwa kuwa
ni ishara ya wananchi kuukubali mradi huo na kuutumia kila siku,
wanapokwenda na kurudi makazini.
Mradi huo unaendeshwa
kwa ubia wa Dart, Kampuni ya UdaRT ambayo ndiyo inaendesha mabasi na
Benki ya NMB ambayo inasimamia upatikanaji wa fedha za mradi huo. Pia,
Maxcom Africa walikuwa wanaendesha mifumo ya kukusanya nauli.
Pia,
mradi huo ambao bado upo kwenye majaribio, unaelezwa wakati mchakato wa
kupanua njia za BRT ili watu wengi zaidi waweze kunufaika
utakapomilika, idadi ya abiria inaweza kuongezeka maradufu.
Hata
hivyo, mabasi hayo yamekuwa yakipata changamoto ya foleni kwenye
makutano ya barabara, Rais John Magufuli aliahidi kuitatua kwa kujenga
barabara za juu.
Tayari, ujenzi wa barabara hizo
unaendelea makutano ya Barabara ya Mandela na Nyerere eneo la Tazara na
Morogoro na Mandela/Sam Nujoma eneo la Ubungo.
chanzo:Mwananchi.
chanzo:Mwananchi.
Comments