
Akizungumza na waandishi wa habari kufuatia tukio hilo huko katika
kituo cha polisi madema Kamanda wa polisi Mkoa wa Mjini magharibi
Kamishna msaidizi mwandamizi wa polisi Hassan Nassir Ali amesema watu
hao wanawake 12 na wanaume 8 wenye umri kuanzia miaka 18.
Kamanda Nassir amesema vijana waliokamatwa walikuwa katika ukumbi wa
hoteli ya Mazson wakiwa katika mafunzo ya kuhamasishana katika vitendo
hivyo. Amefahamisha kuwa jeshi la polisi linaendelea na upelelezi wa
tukio hilo na limesema halitofumbia macho vitendo hivyo ambavyo
vinakwenda kinyume na maadili ya nchi.
Kamanda Nassir amewataka wazazi na walezi kufatilia nyendo za watoto
wao kutojiingiza katika vitendo hivyo ili kuokoa vizazi ambavyo ndio
tegemezi kwa nchi.
Watu hao wamekamatwa katika mafunzo ambayo yameandaliwa na taasisi ya
Bridge Initiative Organization ambayo imesajiliwa Zanzibar kwa lengo la
kutoa elimu ya ukimwi lakini badala yake inahamasisha mapenzi ya jinsia
moja.
chanzo: zanzibar24.
Comments