ZECO linatarajia kuanza kulaza waya umeme unaopita chini ya bahari.

Shirika la umeme zanzibar zeco linatarajia kuanza kulaza waya umeme unaopita chini ya bahari katika kisiwa cha fundo baada kuwasili nchini kutokea china.

Meneja mkuu wa shirika la umeme hassan ali mbarouk akizungumza wakati wa kuangalia waya huo bandarini, amesema waya huo utasafirishwa kesho kutokea bandari ya zanzibar hadi fundo ambapo kazi za ulazaji baharini zitaanza mwishoni mwa wiki hii.


Mradi wa usambazaji umeme katika kisiwa cha fundo umegharimu kiasi cha shilingi bilioni mbili ambazo zimetolewa na serikali ya mapinduzi ya zanzibar huku kazi zote zikiwa zimekamilika ikiwemo ufungaji wa transfoma.

Mradi huo wa kufikisha umeme katika kiswia cha fundo ni utekelezaji wa ahadi ya rais wa zanzibar na mwenyekiti wa baraza la mapinduzi dr. Ali mohamed shein.
chanzo:Zbc.

Comments