Waziri atoa wiki tatu jengo la Mahakama ya mwanakwerekwe kumalizika.

Waziri  wa Nchi  Ofisi ya Rais  Katiba, Sheria, Utumishi wa Umma  na Utawala bora Haroun Ali Suleiman  ametoa wiki  tatu  kwa kikosi cha mafundi wa  KMKM  kukamilisha  ujenzi wa mahakama ya wilaya ya mwanakwerekwe ili kupunguza  msongamano katika mahakama ya kadhi.


Jengo jipya la mahakama ya wilaya ya mwanakwerekwe

Akizungumza  wakati alipotembelea  jengo la mahakama hiyo amesema  kusuasua kwa ujenzi  huo kunapelekea  kukwamisha harakati mbalimbali za watendaji wa mahakama hiyo  jambo ambalo  linalorudisha nyuma shughuli  nyingi za maendeleo.

Waziri Haroun amesema  ameridhishwa  na hatua zilizofikiwa katika ujenzi wa mahakama  hiyo  kujengwa  vyumba vya kutosha, utanuzi wa kumbi za mahakama kwa ajili ya kuskilizia kesi  pamoja na  ofisi za mahakimu.

Muonekano wa Jengo la mahakama ya wilaya ya mwanakwerekwe kabla ya matengenezo
Kwaupande wake  Naibu Mrajisi Mahakama kuu  Zanzibar Khamis Ramadhani Abdalla  amesema  kutokana na uchakavu wa jengo hilo  lilivokuwa awali  serikali kwa makusudi  imeamua kulijenga  upya   ili kunusuru  maisha ya wananchi   kwani lilikuwa katika hali mbaya.

 Amesema jengo hilo lina umuhimu mkubwa  kumalizika kwake  kwani kesi zote zinazotokea katika wilaya ya mjini na magharibi   za   wananchi  zinapelekwa  katika mahakama hiyo ya wilaya  mwanakwerekwe.

 Aidha amesema pia  jengo hilo likiwa katika mazingira mazuri  litaweza kusaidia mahakimu kufanya kazi katika mazingira bora  hasa katika utendaji wa kazi zao.

Zaidi ya Shillingi Milioni Mia moja na thalasini na tano  zimetumika katika ujenzi huo wa mahakama.
Chanzo: zanzibar24.

Comments