
Dk Bokhari ameyasema hayo leo asubuhi alipokuwa akitoa majibu ya
vipimo vilivyochukuliwa hospitalini hapo kwa takriban wiki nzima.
“Vipimo vya damu vimeonyesha kila mtoto ana mfumo wake na hawana
maambukizi ya aina yoyote, ugumu unakuja kwenye ini na moyo ambapo
wanategemeana ila uwezekano wa kutenganishwa upo,” amesema Dk Bokhari.
Majibu hayo yamekuja siku chache baada ya pacha hao kupimwa vipimo
vya radiolojia ikiwemo CT Scan, MRI, X Ray kipimo cha moyo (ECO) pamoja
na vipimo vyote vya damu.
Watoto hao waliozaliwa katika hospitali ya Misheni ya Berega iliyopo
Kanda ya Mashariki mkoani Morogoro, Julai 21 mwaka huu wamenaza
kuchukuliwa vipimo mbalimbali vya awali.
chanzo: zanzibar24.
Comments