Mkurugenzi wizara ya ujenzi, mawasiliano na usafirishaji zanzibar abdallah husein kombo akizungumza katika mkutano wa kuwaelimisha wadau wa mpango wa utafutaji na uokoaji amesema mpango huo kupitia nchi jirani zitasaidiana katika kukabiliana na ajali zinapotokea ili kuharakisha kazi hiyo.
Amesema serikali ya mapinduzi zanzibar imechukua fursa hiyo kuimarisha sekta ya uokozi ili kufanya kazi kwa ufanisi.
Mkuu wa kitengo cha utafutaji na uokoji tanzania norbeth bwire amesema nchi nyingi za afrika bado hazijawa na mipango hiyo hivyo kupitia mpango huo wataimarisha vitengo vya uokozi katika kila nchi husika.
Washiriki wa mkutano huo wamezishauri taasisi zinazohusika na masuala hayo kuimarisha njia za mawasiliano hasa maeneo ya majini pamoja na njia za anga ili kuweza kusaidiana katika uokozi.
Jumuiya ya afrika mashariki iliidhinisha hoja ya utafutaji na uokoaji kupitia kikao cha baraza la mawaziri kilichofanyika juni 2016 ambapo wanatarajia kuridhiwa na nchi wanachama katika kikao kitakachofanyika septemba mwaka huu.
Chanzo:Zbc.
Comments