
Amesema
njia hizo zinatumiwa kwa lengo la kukwepa kukata kibali cha
kusafirishia karafuu jambo ambalo ni kosa kisheria
.
Akizungumza
na wananchi wanaotuhumiwa kujihusisha na vitendo vya ununuzi wa
karafuu , Mkuu wa Wilaya ya Wete Rashid Hadid Rashid ameviagiza vikosi
kuhakikisha mizigo yote inafanyiwa upekuzi ili kudhibiti ujanja
unaofanywa na baadhi ya wananchi.
Mkuu
huyo wa Wilaya amewataka wananchi kushirikiana katika kudhibiti hali
hiyo ili kuiwezesha Serikali kufanikisha azma yake ya kulinda karafuu
dhidi ya wahujumu wa uchumi wanaojali zaidi maslahi yao .
Naye
mkuu wa Jeshi la Polisi Wilaya ya Wete Hamad Omar Suleiman amesema ni
vyema wananchi kufuata sheria bila ya kushurtishwa, ambapo jeshi la
Polisi halitakuwa na huruma na atakayekamatwa akifanya udanganyifu huo .
Wananchi
hao wameahidi kushirikiana na serikali kwa kutoa taarifa sahihi ambazo
zitafanikisha kukamatwa wanaojihusisha na vitendo hivyo ili wachukuliwe
hatua za kisheria lengo ni kukomesha tabia hiyo.
chanzo: zanzibar24.
Comments