
Maombi hayo namba 21 ya mwaka 2017 yametupiliwa mbali na Jaji Wilfred
Dyansobera mapema leo August 11, 2017, baada ya Wakili Mkuu wa
Serikali, Gabriel Malata anayemuwakilisha mdaiwa wa pili Mwanasheria
Mkuu wa Serikali (AG) kusema kesi imeitishwa kwa ajili ya uamuzi.
Katika uamuzi maombi hayo ambayo mdaiwa wa kwanza ni Prof. Lipumba,
Jaji Dyansobera amesema anakubaliana na moja kati ya pingamizi la AG
kwamba vifungu vya sheria vilivyotumika kufungua shauri hilo sio sahihi.
Hata hivyo, amesema anakubaliana na hoja za Bodi hiyo iliyo upande wa
Maalim Seif kwamba suala la Bodi hiyo kutokuwa na uhalali linahitaji
ushahidi wa kina.
Aidha, kuhusu suala la Maalim Seif kusaini hati mbalimbali za shauri
hilo bila kupewa mamlaka, amesema hilo sio pingamizi kwani Mahakama
haiwezi kutoa uamuzi kwa kuangalia kiapo tu.
”Hivyo mahakama imetupilia mbali maombi hayo, kwa sababu
sheria iliyotumiwa kufungua maombi hayo sio sahihi, lakini waombaji
wanaweza kukata rufaa ama kufungua kesi nyingine.”
Baada ya kuelezwa hayo, upande wa Maalim wamesema watafungua upya kesi hiyo.
chanzo: zanzibar24.
Comments