Tathmini
hiyo imebainika kwenye ziara ya Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba Mh.
Omar Khamis Othman wakati akikagua zoezi la ukodishwaji wa mashamba ya
karafuu ya serikali katika bonde la Mtong’ombe shehia ya Mtamwe Kusini
wilaya ya Wete.
Akizungumza
na wananchi hao wakati wa mnada wa ukodishwaji Mh. Omar amewataka
watendaji walioteuliwa kusimamia zoezi hilo kuwa waadilifu na
kuhakikisha hawafanyi upendeleo katika kazi hiyo.
Akitowa
taarifa ya ukodishwaji wa mashamba hayo, Kaimu Afisa Mdhamini wizar ya
Kilimo Maliasili Mifugo na Uvuvi Issa Nassor amesema tayari mashamba 274
yameshakodishwa kwa wananchi.
Msimamizi
wa zoezi hilo Hamad Omar amesema changamoto kubwa inayowakumba ni kwa
wanyeji wa mashamba kutoonesha mipaka halisi ya mashamba hayo.
Zoezi la ukodishwaji wa mashamba ya mikarafuu linaendelea wilaya ya Wete na litafanyika katika wilaya ya Micheweni.
chanzo:Zbc.,
Comments