Daktari feki atoroka na mtoto Hospitali kuu Zanzibar.

Jeshi la polisi mkoa wa mjini magharibi linamshikilia kijana mmoja anaedaiwa kuwa daktari feki katika Hospitali kuu ya Mnazi Mmoja kwakosa la kufanya ulaghai wakimazungumzo pamoja na vitendo na kupelekea kumyakua mtoto.

Kamanda msaidizi, muandamizi wa jeshi la polisi wa mkoa wa mjini magharibi, Hassan Nassir Ali amemtaja kijana huyo, Omar Ali Hajji (29) mkaazi wa Bububu,
kuwa tarehe 31 julai 2017 asubuhi alitaka kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu kutoka kwa mgonjwa aliyefika kupata huduma hospitalini hapo na badala yake kufanya uhalifu wa kumtorosha mtoto.

Kamanda Nassir amefahamisha kuwa mtuhumiwa huyo alidai shilingi elfu kumi kutoka kwa mama wa mgonjwa ili awapatie dawa za matibabu lakini baadae aligundulika kufanya hila ndipo alipokamatwa na kufikishwa polisi.

Akielezea tukio hilo, Mama wa mtoto huyo Mariam Suleiman Hamad amesema baada ya kumpa pesa daktari feki huyo, alimtilia shaka na kuamua kumfuatilia ndipo alipobaini kutaka kutoroka huku akiwa tayari amemchukua mtoto wake.

Aidha Kamanda nassir ametoa wito kwa wazazi wanaofika hospitalini hapo kuwa makini na watoto wao wanaofika nao kwenye hospitali ili kuepuka vitendo vinavyoweza kujitokeza kwa baadhi ya watu amabao hawana imani nzuri na pia kumpongeza mama huyo kwakuwa na hamasa ya kulikabili.

chanzo: zanzibar24.

Comments