ZRB yaja na mfumo mpya wa kulinda kodi za Serikali kwa wafanya biashara.

wafanyabiasharaBodi ya mapato Zanzibar ZRB imewataka wafanya biashara kuwa tayari kuzipokea na kuzitumia mashine za utoaji risiti za mfumo wa kielectroniki (EFB) zinazotarajiwa kufungwa hivi karibuni ili kuondokana na usumbufu wa ukusanyaji wakodi unaojitokeza.

Hii inatokana na kuwepo kwa mfumo wa utoaji wa risiti kwa mkono ambao unaonekana kuwa na matatizo mengi na kupelekea kukosesha Serikali mapato yake.


Akitoa mafunzo kwa waandishi wa habari huko katika kiwanja cha Gombani Chake Chake juu ya matumizi ya Mashine hizo Mkuu wa idara ya sera utafiti na mipango ZRB Nd. Khamis Saadati amesema, utoaji wa risiti kwa kutumia mashine za kielectroniki ni mfumo wa kisasa ambao unatumika katika kutunza kumbukumbu na kuondoa udanganyifu katika ulipaji kodi kwa wafanya biashara.

Amefahamisha kuwa mfumo huo utamuwezesha mteja kupatiwa risiti halali yenye kuonesha uhalali wa bidhaa aliyo nunua pamoja na bei aliyonunulia.

Kwa upande wake Mkuu wa Idara ya Teknolojia ya mawasiliano (ICT) ndugu Mussa Amour Ali amesema, wafanya biashara wanauwezo wa kuichezea mifumo ya zamani ya utoaji risiti na kupelekea kukosekana kwa mapato lakini kwa mfumo huu wa kisasa hautowez a kufanya hivyo kwani mashine hizo zitakuwa zikiendeshwa na ZRB wenyewe.

Amefahamisha kuwa endapo mfanya biashara hatopeleka taarifa za mauzo kwa ZRB basi bodi hiyo itapata ripoti kupitia mashine hiyo.

Mkuu huyo amesema Mashine hizo hawatafungiwa wafanya biashara tu bali maeneo yote hadi kwenye taasisi za Serikali ili kuzuia mwanya wa ukwepaji kodi.
chanzo: zanzibar24.

Comments