
Waziri Mkuu alitoa kauli hiyo alipozungumza kwa nyakati tofauti na
wananchi wa wilaya ya Ruangwa ambapo amesema Serikali imetenga shilingi
trilioni moja kwa ajili ya kusambaza umeme katika vijiji 8,000 ambavyo
bado havijaunganishiwa nishati hiyo.
Waziri Mkuu ambaye ameambatana na mkewe Mama Mary Majaliwa aliyasema
hayo katika mikutano aliyoifanya kwenye vijiji vya Chiapi, Nandanga,
Mbecha na Luchelegwa, ikiwa ni siku ya pili ya ziara yake ya kikazi ya
siku nne Mkoani Lindi.
“Rais wetu Dkt. John Magufuli anajali sana wananchi wake, hivyo
ametenga fedha nyingi zitakazotosheleza kusambaza umeme katika vijiji
vyote vikiwemo na wilaya ya Ruangwa. Gharama za kuunganishiwa umeme huo
ni sh. 27,000 tu.”
Pia Waziri Mkuu amesema mwananchi hawatowajibika tena katika kulipia
nguzo wala fomu za maombi ya kuunganishiwa umeme, kwa sababu tayari
gharama hizo zimeshabebwa na Serikali.
Waziri Mkuu aliongeza kwamba lengo la Serikali ni kufikisha umeme
kwenye vijiji vyote Tanzania na kwa vile ambavyo viko kwenye maeneo
yaliyo mbali na gridi vitafungiwa sola, jambo ambalo litafungua fursa za
ajira na kukuza uchumi.
Waziri Mkuu alisema huduma hiyo ni muhimu kwani mbali ya kutumiwa
majumbani lakini pia kwa kusogezwa karibu na maeneo ya pembezoni
itawezesha zahanati,shule ,viwanda na vituo vya afya kuwa na umeme.
Kwa upande wake Meneja wa Tanesco Mkoa wa Lindi Mhandisi, Johnson
Mwigune alimuhakikishia Waziri Mkuu kwamba hadi kufikia mwishoni mwa
mwezi huu mkandarasi aliyepangiwa katika vijiji hivyo atakuwa tayari
ameanza kazi ya kusambaza umeme.
chanzo: zanzibar24.
Comments