Wananchi wa Zanzibar changamkieni fursa za kimaendeleo.

Wananchi  wametakiwa  kuchangamkia fursa  zilizopo  katika  kampuni ya Fumba Town development  ambazo zitakazoweza  kuwapatia ajira na kupata  huduma nyengine za kijamii.

Akizungumza na Waandishi wa habari  huko ofisini kwake mazizini Afisa Mtendaji wa kampuni hiyo Tobias Dietzold amesema  tokea kuanzishwa mradi wa Fumba wa kujenga nyumba pamoja na mambo mengine ya maendeleo  muitiko kwa wananchi umekuwa mdogo kujitokeza kuomba nafasi  za ajira na kuwahimiza wananchi kujitokeza ili kuweza kushiriki katika shughuli mbalimbali za kimaendeleo.

Hata hivyo amesema  mradi huo  utaweza  kuwanufaisha wananchi katika Nyanja za maendeleo   lengo ni kuboresha maisha ya watu kimakaazi pamoja na kuweka huduma za kijamii katika maeneo ya nyumba hizo ambazo zitawanufaisha wananchi walio wengi ikiwemo skuli,hospitali ya kisasa pamoja na huduma ya maji safi na salama.
Amesema  tokea kuanzishwa mradio huo oktoba  mwaka 2015 hadi mwaka huu2017 nyumba takribani 80 za ghorofa zimekamilika na malengo ya mradi huo ni kujenga nyumba Elfu 1020.
chanzo:Zanzibar24

Comments