Akizungumza wakati wa kukabidhi vifaa vya ujenzi wa maendeleo katika jimbo hilo walivyo vitoa kwa kushirikiana na mbunge wa jimbo makame ma shaka fumu mh: makungu ambae ni naibu waziri wizara ya ardhi , maji , nishati na mazingira amesema ushirikiano ndio njia pekee ya kuinua maendeleo ya wananchi hivyo ni vyema kwa kila mwananchi kutoa taarifa kwa viongozi wao wakiwa na matatizo.
Amesema lengo la serikali ni kuhakikisha huduma za kijamii zinawafikia wananchi wote bila ya kujali itikadi zao za kisiasa, dini na kabila jambo ambalo limefikiwa kwa kiwango kikubwa.
Kwa upande wake mbunge wa jimbo hilo amesema serikali zote mbili zinatekeleza ilani ya chama cha mapinduzi hivyo watakuwa tayari kusimamia kwa makini masuala ya kimaendeleo ili kuhakikisha malengo ya serikali zote yanafanikiwa.
Nao wananchi wa jimbo hilo wamesema walikuwa wanapata usumbufu mkubwa katika upatikanaji wa maji safi na salama, miundo mbinu pamoja na uhaba wa matundu ya vyoo hivyo watahakikisha misada hiyo itatumika ipasavyo.
Miongoni mwa misaada iliyotolewa na mbunge na mwakilishi ni mashine za maji katika vijiji vya kivunge, michenzani pita na zako, pita nazako michenzani , mifuko kumi ya saruji kwa tawi la ccm kivunge bondeni pamoja na matofali 1300 kwa ajili ya ujenzi wa vyoo skuli ya sekondari potoa.
chanzo:Zbc.
Comments