Wanafunzi wa vyuo vikuu kuacha tabia ya kufanya udanganyifu.

Mkuu wa wilaya ya kusini unguja ndugu idrissa kitwana amewaagiza wanafunzi wanaojiunga na vyuo vikuu ndani na nje ya zanzibar kuacha tabia ya kufanya udanganyifu wakati wanapoomba mikopo.

Amesema tabia ya kufanya udanganyifu katika vyeti halitowafikisha pahala wanapopataka pa kuelekea elimu ya juu.


mkuu huyo wa wilaya ametoa agizo hilo wakati akifungua mafunzo ya udakhili yanayofahamisha juu ya namna ya kujinga na vyuo vikuu tanzania yaliyofanyika skuli ya haileselasie.

Amewataka wanafunzi hao kuzitumia nafasi wanazopata pamoja na kujiamini wakati w a kuchagua masomo wanayyoombea mikopo.

Mkuu wa kitengo cha udakhili kutoka nacte twaha twaha amewakumbusha wanafunzi hao kwamba wanapokoseshwa mikopo huku wakiwa na sifa kwamba wanahaki ya kukata rufaa ya kujiunga.

Mwenyekiti wa umoja wa vyuo vikuu zanzibar zamil juma simai amesema mafunzo hayo yatasadia wanafunzi kujua sifa zinazostahiki na zisizo stahiki kuiunga na vyuo vikuu ili kupunguza malalamiko baada ya kukosa kujiunga.
chanzo:Zbc.

Comments