Wanafunzi kuyapa kipaumbele masomo ya sayansi.

Wanafunzi wamesisitizwa kuyapa kipaumbele zaidi masomo sayansi ili kukabiliana na tatizo la uhaba wa masomo hayo maskuli na uhakika wa kupata ajira.

Waziri wa elimu na mafunzo ya amali mh; riziki pembe juma ametoa kauli hiyo katika skuli ya donge’ wakati akipokea vifaa kutoka shirika la kinder hut foundation .


Riziki pembe amesema hivi sasa wizara yake inakabliwa na upungufu mkubwa wa walimu wa masomo hayo na hivyo kusababisha wanafunzi kutofanya vizuri katika masomo yasayansi.

Akisoma risala kwa niaba ya walimu wezake mwalim raya mashauri amesema kwakipindi chote kilichopita skuli hiyo imekabiliwa na matatizo mbali mbali lakini kupatikana kwa vifaa hivyo kutasaidia harakati mbali mbali ambazo zinahitajika kwao wao na wanafunzi kwa ujumla.

Kutokana na hayo yote nao wanafunzi wa skuli ya donge hawakusita kupokea vifaa hivyo na kusema hifaa hivyo vitawasaidia katika kujisomea zaidi na kufikia malengo yao ya kimasomo.

Wafazili hao licha ya kutoa msaada pia wameboresha laibrari, chumba cha maabara ambapo skuli ya donge ni skuli moja wapo imeanzishwa mwaka 1930 ambapo hivi sasa ina miaka 87.

chanzo:Zbc.

Comments