
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Sudan Kusini Jenerali Taban Deng Gai
ameeleza taifa lao linataka kufundisha lugha ya kiswahili katika shule
mbalimbali nchini humo.
maombi hayo ameyatoa wakati alipo kutana na kufanya mazungumzo na
Makamu wa Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kando ya Mkutano wa 29
wa Wakuu wa Nchi na Serikali ya Umoja wa Afrika Jijini Addis Ababa
Ethiopia.
Pia Jenerali Taban Deng ametoa shukurani kwa Serikali ya Tanzania kwa
kuiunga mkono Serikali ya Sudan Kusini kupitia Jumuiya mbalimbali
hususan Jumuiya ya Afrika Mashariki katika harakati zake za kupambania
amani ya kudumu sambamba na kuwavumilia kipindi chote wanapopitia
changamoto kufikia amani hiyo.
Kiongozi huyo amesema taifa lao bado ni changa barani Afrika hivyo
ipo haja Serikali ya Tanzania kulisaidia ili liweze kuimarisha
kiulinzi na usalama pamoja na uimarishaji wa utoaji wa huduma za msingi
kwa wananchi wake.
Nae makamo wa rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amesema ili
Tanzania iweze kushirikiana vizuri na Serikali ya Sudan Kusini ni lazima
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushikiriano wa Kimataifa za nchi hizo Mbili
kuandaa mfumo maalum wa ushirikiano na utekelezaji wake.
Mfumo utakao ainisha maeneo ya kushirikiana katika sekta tofauti
ikiwa katika sekta za afya, elimu, kilimo, siasa, ulinzi na usalama nk.
chanzo: zanzibar24.
Comments