Taarifa ya pamoja ya Chama cha Wanasheria wa Afrika Mashariki, SADC na Pan African kuhusu kukamatwa kwa Rais wa TLS, Tundu Lissu.
Wakati
wenzao wakisema makosa manne ndiyo yanayoweza kumlazimu mtuhumiwa
kupimwa mkojo, Jumuiya ya Afrika Mashariki imesema inafuatilia sakata la
mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu anayeshikiliwa na Jeshi la
Polisi.
Lissu, ambaye ni Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), alikamatwa Alhamisi akiwa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) wakati akisubiri kwenda Kigali, Rwanda kuhudhuria mkutano wa jumuiya hiyo.
Wanasheria
wa Lissu wamesema waliambiwa na polisi kuwa amekamatwa kwa tuhuma za
uchochezi, lakini alitakiwa kutoa kipimo cha mkojo, jambo ambalo limezua
maswali.
“Tutafanya
mipango ya kufuatilia kesi ya Wakili Tundu pamoja na mchakato mwingine
wowote wa mahakama ambao umeshafikishwa mahakamani au unaweza kufikishwa
mahakamani, kwa niaba yake kuthibitisha haki za Mtanzania kama
zilivyoelezwa na sheria ya kimataifa,” inasema taarifa ya Chama cha Wanasheria wa Afrika Mashariki (EALS) iliyosainiwa na rais wake, Richard Mugisha.
Taarifa
hiyo pia imeeleza kuwa EALS inachukulia kukamatwa kwa Lissu kama ishara
nyingine ya kuendelea kuzorota kwa uhusiano baina ya Serikali na TLS,
hali iliyoanza wakati wa uchaguzi wa viongozi wa chama hicho.
“Ni
kitu kilicho wazi kuwa uhusiano huo umekuwa ukiharibika tangu kipindi
cha kuelekea na baada ya matokeo ya Mkutano Mkuu wa mwaka wa TLS ambao
Wakili Lissu alichaguliwa na wanasheria wenzake kuongoza TLS kwa mwaka
mmoja,” anasema Mugisha.
Wakati
EALS ikitoa msimamo huo, wanasheria nchini bado wanahoji sababu za
Lissu kuchukuliwa kipimo cha mkojo wakati akituhumiwa kwa makosa ya
uchochezi.
Kwa
mujibu wa wanasheria hao, makosa yanayoweza kusababisha mtuhumiwa
achukuliwe kipimo hicho ni ya usalama barabarani, matumizi ya dawa za
kulevya, ubakaji na mashauri ya ndoa na watoto ambayo hulazimu mkemia
kupima sampuli hizo.
Lakini
Msemaji wa Jeshi la Polisi, Barnabas Mwakalukwa alisema uchunguzi wa
polisi hauna mipaka na kwamba jeshi hilo halifanyi kazi kwa mihemko ya
watu, bali kwa kuzingatia weledi.
Alisema
kitendo cha watu kuhoji suala la Lissu kupimwa mkojo ni kuingilia
uchunguzi. Alisema uchunguzi ni suala pana, hivyo kuwataka wasubiri
mtuhumiwa huyo atakapofikishwa mahakamani na kusomewa mashtaka yake.
“Kwenye
suala la ku-suspect (kutuhumu), polisi anaweza ku-suspect anything
(kitu chochote) kutoka kwa mtu yeyote. Siwezi kuelezea mikakati na mbinu
za kiuchunguzi, lakini mtambue kwamba uchunguzi is too general (ni
mpana), unaweza kuchunguzwa kwa mambo mengi,” alisema Mwakalukwa.
==>Hapo chini kuna tamko la Wanasheria Hao
==>Hapo chini kuna tamko la Wanasheria Hao
chanzo:Mpekuziblog.
Comments