Serikali ya Ujerumani imetiliana saini na Serikali ya Mapinduzi ya
Zanzibar mkataba wa utengenezaji wa ujenzi mpya wa majumba ya mjerumani
kikwajuni mjini Zanzibar ili kuziendeleza nyumba hizo kuwa
katika mazingira bora ya kuishi.
Akizungumza katika hafla hiyo ya utiaji saini Mstahiki meya wa Mji
wa Potsdam Ujerumani Jann Jakobs amesema uimarishajwi wa nyumba hizo ni
muendelezo wa uhusiano mwema uliopo kati ya Zanzibar na ujerumani
katika kuwaletea wananchi maendeleo.
Hata hivyo amesema mbali na ujenzi wa nyumba hizo lakini pia
Ujerumani imekusudia kusaidia Zanzibar katika sekta za maendeleo
ikiwemo sekta ya Elimu, Afya katika kitengo cha Kensa na mazingira.
Kwaupande wake Mstahiki meya wa Zanzibar Khatib Abrahmani Khatib
amesema uhusiano huo utaweza kuinua fursa za kiuchumi kati
ya Manispaa ya mji wa Zanzibar na jiji la Potsdam Ujerumani ili kuweza
kunufaika na miradi mbalimbali ya maendeleo.
Aidha Mstahiki huyo
amesema ili kudumisha ushirikiano uliopo wataandaa mikakati ya
pamoja ili kurahisisha mawasiliano kati yao na uhamasishaji wa vikundi
vya vijana kushiriki katika ujenzi huo kupata ajira.
chanzo:zanzibar24.
Comments