Akizungumza na Zanzibar24 nje ya mafunzo kwa wanafunzi mbalimbali Unguja na Pemba yaliyofanyika katika uwanja wa baraza la wawakilishi
la zamani kikwajuni Mwenyekiti wa taasisi ya Afrika Malaika Fiona
Barretto amesema watoto wa kike bado wapo nyuma kujifunza katika masomo
ya sayansi na teknolojia jambo linalochangia kuonekana hawana
uwezo na kushindwa kupewa nafasi hasa katika uongozi.
Hata hivyo amesema endepo wasichana wakizembea kutumia fursa
hizo za kujifunza hawata songa mbele kimaendelo lengo la mafunzo
hayo ni kumpa kipaumbe msichana kujifunza masuala ya sayansi na
teknolojia ili kwenda sambamba na hali ya maisha na uchumi wa viwanda.
Kwaupande wake Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Riziki
Pembe Juma Akizungumza na Zenji fm radio mara baada ya kutembelea na
kukagua mafunzo hayo amesema ujio wa taasisi hiyo nifaraja kubwa
kwa walimu na wanafunzi kwani mafunzo hayo yatamjenga mwanafunzi wa
kike kuwa na moyo wa kusoma masomo ya sayansi ili kufikia malengo.
Aidha Pembe ametoa wito kwa wanafunzi hasa wakike kusoma zaid masomo
ya sayansi ili kupata ujuzi wa kutosha utakaowasaidia baadae katika
maendelo yao.
Zaidi ya wanafunzi mia 400 wamepatiwa mafunzo ya hesababi , sayanasi na teknolojia pamoja na Kingereza.
Chanzo: Zanzibar24
Comments