
Maneno hayo yemesemwa na kamanda wa Polisi Mkoa wa kusini Unguja
kamishna msaidizi wa Polisi Juma saidi Khamis baada ya kijana Ame
Mwadini Nahoda mwenye umri wa miaka 19 mkaazi wa Kichaka Mabundi Mwera
shehia ya ubago amembaka msichama wa miaka 20 ambae ni mlemavu wa miguu
na pia ni bubu.
Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo kamanda Juma Saidi
Khamis amesema tukio hilo la kusikitisha limetoke Jully 12, 2017 majira
ya saa tano asubuhi na kuripotiwa kituo cha polisi dunga.
“Kumbaka mwanamke ambae ni mlemavu nikosa kubwa kisheria na
mpaka sasa mtuhumiwa tumesha mkamata na tunakamilisha taratibu za
upepelezi ili jalada tulipeleke kwa mkurugenzi wa mashta kwa ajili ya
hatu za mahakamani” alisema msaidizi wa kamishna wa Polisi Juma.
Nae Mratibu wa wanawake na watoto katika shehia ya Ubago Mwajuma
Hassan Abdallah imeomba jamii kuto ficha vitendo hivyo ili sheria ziweze
kuchukuliwa.
Mtuhumiwa watukio tukio hilo anatarajiwa kufikishwa mahakamani pale tu upelelezi utakapo kamilika.
chanzo:zanzibar24.
Comments