Mganga wa Kienyeji ahukumiwa miaka 30 jela Dar es salaam.

Mganga wa kienyeji akitambulika kwa jila la Wilson Mkomi mwenye umri wa miaka 30 afunguliwa mashtaka katika mahakama ya kinondoni kwa kesi ya ubakaji.

Mahakama hiyo imemtia hatiani Mshtakiwa na kumuhukumu kifungo cha miaka 30 jela katika kosa la ubakaji ambalo alilitenda December 29, 2016 maeneo ya Kawe Ukwamani, Kinondoni.


Hukumu hiyo imetolewa na Hakimu wa Mahakama hiyo Joyce Mushi ambapo alisema mshtakiwa ametiwa hatiani kwa kosa la ubakaji hivyo anahukumiwa kifungo cha miaka 30 jela.

 chanzo:zanzibar24.

Comments